14 Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.

15 Kama mguu ungejisemea: "Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili", je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!

16 Kama sikio lingejisemea: "Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili", je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!

17 Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?

18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.

19 Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?

20 Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.