5 Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi--ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi.6 Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha.7 Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa.8 Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda.
publicidade