1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na walimu; miongoni mwao akiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.

2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema: "Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia."

3 Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.