13 Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.

14 Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ngombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.

15 Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ngombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.

16 Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, "Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!"

17 Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: "Upendo wangu kwa nyumba yako waniua."