28 Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe."29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini?30 Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema.31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu.
publicidade