25 Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, "Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?"
26 Yesu akamwuliza, "Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?"
27 Akamjibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe."
28 Yesu akawaambia, "Vema! Fanya hivyo, nawe utaishi."