11 Mtoto akimwomba baba yake samaki, je, atampa nyoka badala ya samaki?
12 Na kama akimwomba yai, je, atampa nge?
13 Ninyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri. Basi, baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba."