38 Hapo, mtu mmoja katika lile kundi akapaaza sauti, akasema, "Mwalimu! Ninakusihi umwangalie mwanangu--mwanangu wa pekee!

39 Pepo huwa anamshambulia, na mara humfanya apige kelele; humtia kifafa, na povu likamtoka kinywani. Huendelea kumtesa sana, asimwache upesi.

40 Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza."

41 Yesu akasema, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini?" Kisha akamwambia huyo mtu, "Mlete mtoto wako hapa."

42 Wakati mtoto huyo alipokuwa anamjia Yesu, yule pepo alimwangusha chini na kumtia kifafa. Lakini Yesu akamkemea yule pepo mchafu akamponya mtoto na kumkabidhi kwa baba yake.

43 Watu wote wakashangazwa na uwezo mkuu wa Mungu. Wale watu walipokuwa bado wanashangaa juu ya mambo yote aliyofanya, Yesu aliwaambia wanafunzi wake,