3 "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.6 Jua lilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.8 Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia."9 Kisha akawaambia, "Mwenye masikio na asikie!"
publicidade