48 Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea akitembea juu ya maji. Alitaka kuwapita.

49 Lakini walimwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu, wakapiga yowe.

50 Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!"

51 Kisha akapanda mashuani walimokuwa, na upepo ukatulia. Nao wakashangaa sana.