publicidade

Mateus 13

3 naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.6 Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.8 Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini.9 Mwenye masikio na asikie!"

publicidade