13 Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, "Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?"
14 Wakamjibu, "Wengine wanasema kuwa ni Yohane mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii."
15 Yesu akawauliza, "Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?"
16 Simoni Petro akajibu, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai."