26 Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, "Twaeni mle; huu ni mwili wangu."

27 Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema, "Nyweni nyote;

28 maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano,*fn* damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi.

29 Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu."

30 Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.