10 Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja Sheria yote.

11 Maana yuleyule aliyesema: "Usizini," alisema pia "Usiue". Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.

12 Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru.