9 Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

10 Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.

11 Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?

12 Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.